![]() |
| OGBU (KULIA) AKIWA KAZINI NA TIMU YAKE YA HEARTLAND.... |
Alhamisi, Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pillars FC ya Nigeria ambayo inaundwa na wachezaji kutoka timu mbalimbali. Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Ogbu ni mshambuliaji wa Heartland ya Nigeria ambayo ni moja ya timu kubwa nchini humo na amekuwa tishio kwa upachikaji mabao kwa misimu miwili iliyopita.
Brandts amesema Ogbu ili apate nafasi ya kumuona na mechi ya pili itakuwa ni ile dhidi ya URA ya Uganda itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
“Kwanza ataanza mazoezi na sisi Jumatano, halafu Alhamisi nitampa nafasi katika mechi ya kirafiki. Lakini baadaye nitampa nafasi tena Jumapili tutakapocheza na timu ya Uganda.
“Bado ni mchezaji ambaye anatakiwa kuangalia, hivyo ningeshauri benchi la ufundi tupewe nafasi kwanza,” alisema.
Mnigeria huyo ametua usiku wa kuamkia leo tayari kufanya majaribio ya kujiunga na Yanga.








0 COMMENTS:
Post a Comment