July 16, 2013


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ametoa mpya kwa kuwatishia kuwafuta uanachama wanachama wa klabu hiyo watakaozungumza kwenye vyombo vya habari.
Rage ‘raia’ wa Tabora ametoa kali hiyo leo kwa kusema mwanachama atakayefanya hivyo, atafutwa uanachama mara moja.

Wanachama waliokuwa wakihojiwa na Redio One kutokea jana walilalama kuhusiana na uamuzi wa uongozi wa Rage kuitisha mkutano wa wanachama ndani ya siku 15.

Wanachama hao walisema uongozi wa Rage umeikanyaga katiba ambayo inaangiza mkutano kuitishwa ndani ya siku 90.



Kutokana na kulaumu kwao, Rage alisisitiza mkutano huo utafanyika Juni 20 kama ulivyopangwa na mwanachama atakayesikika anazungumza redioni atafungiwa.

Ingawa hakuna kipengele chochote katika katiba ya Simba kinachosema mwanachama atafutwa uanachama kwa kuzungumza kwenye chombo cha habari, Rage alisisitiza hilo.

“Hata mimi ni mbunge hivyo siwezi kuzungumza mambo ya bunge nje ya bunge, mfano nianze kumsema spika nje badala ya kufikisha malalamiko yangu bungeni,” alisema.


Uongozi wa Rage umekuwa ukilalamikiwa na wanachama kuendesha mambo kiujanjaujanja lakini mwenyewe amekuwa mbabe na asiyetaka kukosolewa hata kidogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic