Pamoja na kuwa gumzo la usajili, Luis Suarez amelamba tangazo la benki ambalo ameigiza kama mfanyakazi na baadaye anajiangusha kama ambavyo amekuwa akilalamikiwa uwanjani.
Suarez amekuwa akilalamikiwa katika Ligi Kuu England kwamba ana tabia ya kujiangusha anapokuwa anaichezea Liverpool.
Katika tangazo hilo la Bank Abitab ya Uruguay, Suarez anaonekana akiwa bize na wafanyakazi wenzake na baadaye anajirusha kama ambavyo amekuwa akianguka uwanjani.
Tangazo hilo la benki linaonekana kuwa na vichekesho vingi na Suarez ni sehemu kubwa ya kuvutio.
Pamoja na kutakiwa na Real Madrid kwa udi na uvumba, Liverpool imemtangaza kuwa ni kati ya wachezaji wake wanaokwenda katika ziara katika nchi za Indonesia, Thailand na Australia.










0 COMMENTS:
Post a Comment