Kijana mmoja ameweka rekodi mpya baada ya kulikimbiza basi la wachezaji wa Arsenal kwa maili tatu.
Arsenal iko katika ziara barani Asia na kijana huyo alifanya hivyo wakati timu hiyo maarufu ilipokuwa nchini Vietnam.Kijana huyo anavutiwa sana na Arsenal na zaidi wachezaji hawa; Theo Walcott na Jack Wilshere, hivyo alikuwa akilikimbiza basi hilo ili kupata saini zao.
Akiwa amevaa jezi ya Arsenal, kijana huyo aliendelea kulikimbiza basi hilo hadi akafikia kuanguka baada ya kujigonga katika nguzo ya barabarani.
Bwana mdogo huyo amekuwa shabiki mwenye bahati zaidi wa Arsenal mwaka huu, kwani baadaye basi lilisimama akapata bahati ya kuingia ndani na kupiga picha na wachezaji kadhaa.
Lakini kichekesho zaidi wachezaji walianza kumuona Kocha Arsene Wenger amsaini bwana mdogo huyo kwa kuwa pamoja na kuonyesha ana mapenzi makubwa na Arsenal lakini ana pumzi ya kutosha hata kucheza kiungo.









0 COMMENTS:
Post a Comment