![]() |
| OKWI AKIITUMIKIA ETOILE DU SAHEL (PICHA: ESS, RUHUSA KWA SALEHJEMBE BLOG) |
Klabu ya Etoile Du Sahel umeitaka Simba
kufanya mchakato wa kumuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi ili iweze kurejesha
gharama zake za dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 480) inazodai.
Uamuzi huo wa Etoile Du Sahel umetokana
na tabia ya Okwi kuchelewa kurejea kazini kila anapopewa nafasi ya kwenda
kuitumikia timu yake ya taifa ‘The Cranes’.
Katibu Mkuu wa Etoile Du Sahel, Adel
Gith amesema kuwa wamejitahidi kadiri ya uwezo wao lakini inaonekana mchezaji huyo
ni tatizo katika suala la nidhamu na hawezi kupata soko sehemu yoyote duniani
hasa kwa watu makini.
“Inawezekana kuna sehemu nyingi ambayo
alikuwa anatakiwa kabla ya kuja hapa, Simba wanaweza kuwa wanajua ndiyo maana
baada ya kuja hapa tuliwaambia kuwa wamuuze halafu wachukue fedha yao,”
alisema.
“Lakini wao walisisitiza kuwa wanataka
fedha ingawa walituambia wakisikia anatakiwa sehemu, basi watatusaidia. Lakini
inaonekana hapa hatakuwa na nafasi, hawezi kuwa mchezaji anayekaa nje timu kwa
zaidi ya wiki bila ya taarifa na hapokezi simu za viongozi,” alisema.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza
uongozi wa Msimbazi ulisisitiza kuwa hauhusiki na suala la kuuzwa, kwanza ni
fedha wanazodai na biashara nyingine ifuatie.
“Unajua alikwenda Katibu Mkuu (Evodius)
Mtawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili (Zacharia) Hans Pope. Wao
walisisitiza kwamba wanachotaka ni fedha kwanza, suala la kusaidiana kumuuza
litafuatia,” alisema.
Kwa upande wa uongozi wa Simba, Mtawala
alisema wanachojua wanawadai Etoile Du Sahel, wanachotaka ni kulipwa fedha zao
tu.
“Kwanza kabisa ni fedha, kama
watashindwa tutalifikisha hili suala Fifa.
Biashara ya kumuuza Okwi si kazi
yetu kwa kuwa ni mchezaji wao,” alisema Mtawala huku akisisitiza Simba sasa
haiko katika nafasi ya kulizungumzia kwa urefu suala hilo.








0 COMMENTS:
Post a Comment