July 25, 2013


JAVU AKISHANGILIA BAADA YA KUITUNGUA YANGA MJINI MOROGORO MSIMU ULIOPITA..


Mshambuliaji nyota wa Mtibwa Sugar, Hussein Javu ametua Yanga na kuanza mazoezi na timu hiyo.

Javu alikuwa mwiba kwa Yanga msimu uliopita baada ya kufunga mabao katika kila mechi Mtibwa waliyokutana na Yanga.

Taarifa zinaeleza Javu amemalizana kila kitu na Yanga na leo asubuhi alitarajia kuanza mazoezi.

Hata hivyo, dau limekuwa likifichwa sana na mmoja wa viongozi wa Mtibwa Sugar alisema walimalizana juzi usiku.

“Hili wanaweza kulizungumzia Yanga wenyewe, lakini Javu ataanza mazoezi Alhamisi asubuhi ndiyo nimesikia hivyo,” alisema kiongozi huyo.
Yanga ilianza kumuwania Javu  miezi miwili iliyopita, lakini ilionekana kama Mtibwa Sugar wameweka dau kubwa sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic