July 25, 2013




Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto ameonekana katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam na kuzua taharuki.

Kazimoto alitoroka katika kambi ya timu ya taifa na kuelezwa kuwa alikimbilia Qatar kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Lakini kuna taarifa, Kazimoto amemueleza rafiki yake wa karibu kwamba hakwenda Qatar na badala yake alijichimbia jijini Dar, kimyaa.

“Anasema kuna mtu alimkasirisha sana katika timu ya taifa, akaamua kujiondoa na kukaa pembeni.


“Mwinyi si mtu wa maneno mengi, hivyo aliamua kukaa kimya tu kuacha watu waseme wanachotaka,” alisema rafiki yake huyo na kuongeza.

“Ndani ya siku chache huenda akajiunga na kambi ya Simba iliyoko Bamba kama hakutakuwa na tatizo.”

Tayari TFF imeishatangaza kuwa itamchukulia hatua kutokana na kitendo cha kutoroka kambini na kulazimisha Kocha Kime Poulsen kumuita kinda, Mudathir Yahya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic