STARS WAKIWA NA MAZOEZI YA MWISHO KWENYE UWANJA WA MANDELA MJINI KAMPALA...TAYARI KIKOSI HICHO KIMETUA UWANJANI HAPO TAYARI KWA MECHI YA LEO |
Daktari
wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mwanandi Mwankemwa ameilalamikia hoteli ya Mount
Zion iliyopo, Kampala, Uganda ambayo wametayarishiwa na wenyeji wao The Cranes,
kwa kuwapa chakula kiduchu na ambacho hawaendani nacho na kusema hizo ni mbinu
za wenyeji wao, The Cranes kutaka kuwamaliza.
Akizungumza
na Championi, Mjini Kampala Dk. Mwankemwa amesema: "Jana Alhamisi
ulipofika muda wa chakula cha jioni walituandalia kajichakula kama ka'mtoto na
kusema eti hiyo ndiyo futari waliyotuandalia" alilalamika Mwankemwa.
Dk
Mwankemwa alisema katika futari hiyo waliandaliwa uji, tambi na ndizi kidogo na baada
ya wachezaji kupewa chakula hicho yaliyokea malumbano makali ya kupunjwa msosi
wachezaji walilalamikia sana hivyo ikabidi amfuate Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo,
Onesmus Masingazi na kumlalamikia.
Baada ya
kumpelekea meneja huyo malalamiko hayo, meneja huyo alijaribu kusisitiza kuwa
hivyo ndivyo alivyopangiwa kufanya na mabosi wake lakini baada ya malumbano
kuzidi alikubali kuwabadilishia msosi siku inayofuata na kuahidi kuwaongeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment