July 25, 2013



 
TATA BAADA YA KUTUA BARCELONA, LEO

Kocha mpya wa Barcelona, Gerardo 'Tata' Martino tayari ametua Barcelona kwa ajili ya kusaini mkataba na klabu yake hiyo mpya.

Kocha huyo maarufu kama Tata amewasili leo jijini humo na alikutana na Mkurugenzi wa soka wa Barcelona, Andoni Zubizarreta.
 
TATA KABLA YA KUONDOKA ARGENTINA..

Kabla ya kuondoka nchini Argentina, kikundi cha mashabiki wachache wa Newells Old Boys kilijitokeza kikiwa na bango lililoandikwa “Kilometa 13,000 zimetutenganisha”. Wakiwa na maanda umbali kutoka Argentina hadi Hispania.


Kocha huyo atakutana na kikosi chake kwa mara ya kwanza nchini Norway wakati Barcelona itakapocheza mechi yake ya pili ya kirafiki baada ya kulala mabao 2-0 mjini Munich.

Mbele ya Tata, Barcelona itachea mechi ya kirafiki dhidi ya Valerenga na kipute hicho kitapigwa Jumamosi jijini Oslo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic