Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema uongozi wao unajua alipo kiungo Mwinyi Kazimoto na si hapa nchini.
Pamoja na Kamwaga kushindwa kusema alipo Kazimoto, lakini blogu hii imegundua bado yuko nchini Qatar ambako anaendelea na majaribio.
“Sisi tunajua alipo, lakini hatuwezi kuzungumza lolote kwa kuwa aliondoka akiwa katika mikono ya timu ya taifa,” alisema.
Lakini Mtanzania mwingine anayeishi nchini Qatar amethibitisha kuwa leo mchana, Kazimoto amekuwa akiendelea na majaribio.
“Aliyesema amerudi Dar anawapotosha, Kazimoto bado yuko huku,” alisema Mtanzania huyo.
Leo asubuhi magazeti matatu yaliripoti kuonekana kwa Kazimoto jijini Dar es Salaam.
Lakini rafiki mmoja wa Kazimoto naye akasema kiungo huyo wala hakwenda Qatar na badala yake yuko nchini.
Hali hiyo imekuwa ikizua mkanganyiko mkubwa kuhusiana na alipo Kazimoto tokea alipotoroka nchini na kwenda Qatar.
0 COMMENTS:
Post a Comment