Kinda Brendan Ogbu ametua nchini tayari kujiunga na Yanga kwa ajili ya kuichezea msimu ujao.
Ogbu raia wa Nigeria ni kati ya wachezaji nyota wanaotisha katika ushambuliaji akiwa na klabu yake ya Heartland ya Nigeria.
Ameamua kuja nchini kujiunga na Yanga na kesho asubuhi ataanza mazoezi akiwa na timu hiyo ili kumuonyesha Kocha Ernie Brandts kazi yake.
Lakini kuna mambo kadhaa huenda unataka kuyajua kuhusiana na Ogbu na 10 kati ya hayo ni haya;
Moja:
Mara ya kwanza kufunga mabao mengi katika Ligi Kuu ya Nigeria ilikuwa ni msimu wa 2010-2011 wakati mshambuliaji huyo alipoifungia timu yake ya Enugu Rangars mabao tisa.
Mbili:
Msimu wake wa kwanza kabisa na Ligi Kuu ya Nigeria ilikuwa ni mwaka alipjiunga na Enugu Rangers akitokea klabu ndogo ya UNTH FC. Akaonyesha ni mkali, hiyo ilikuwa ni msimu wa 2008-2009, akafunga mabao mawili tu.
Tatu:
Msimu wa 2009-2010 wa Ligi Kuu ya Nigeria akiwa na Enugu Rangers ndiyo ulikuwa mbaya zaidi kwake, kwani pamoja na kucheza zaidi ya mechi kumi alifunga bao moja tu.
Nne:
Januari, 2011, Ogbu aliteuliwa kuwa mchezaji kinda aliyeonyesha kiwango kizuri zaidi na akaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya miaka 20 akiwa mmoja wa wachezaji wachache wanaocheza nchini Nigeria waliopata nafasi hiyo.
Tano:
Kumekuwa na utata kuhusiana na umri wa mshambuliaji huyo ambaye inaelezwa ana umri wa miaka 20 sasa, lakini mwaka 2011 kuna wakati ilielezwa ana miaka 18 lakini upande mwingine ukazua zogo akiwemo baba yake mzazi baada ya kueleza alikuwa na miaka 15.
Sita:
Ogbu ni kati ya mwanasoka anayetokea katika familia ya wanamichezo kwa mujibu wa MTN Football, baba yake mzazi ni amekuwa mchezaji wa kimataifa wa mpira wa mikono wakati mama yake pia amekuwa mchezaji wa kimataifa wa Nigeria wa mpira wa kikapu.
Saba:
Ogbu amekuwa ndiye mwanasoka ambaye jina lake linachanganywa zaidi na mitandao ya Kinigeria kuliko mwingine yoyote. Wengi wamekuwa wakichanganya namna hii; ”Bertrand Ogbu”, ”Bernard Ogbu”, ”Brenthran Ogbu” na ”Brenda Ogbu”.










0 COMMENTS:
Post a Comment