Beki nyota
wa zamani wa Simba, George Magere Masatu amerejea nchini baada ya kuishi
ughaibuni kwa zaidi ya miaka 10.
Masatu
alikuwa kicheza soka la kulipwa nchini Indonesia lakini baadaye akastabu na
kuamua kufanya kazi ya ukocha.
Masatu
alifanya kazi kwa miaka mitatu na ushee akiwa mwalimu katika kituo cha watoto
wadogo kilicho chini ya Arsenal ya England.
Akiwa
Indonesia amekuwa akifanya kazi katika kituo hicho kwa kushirikiana na makocha
wengine wakiwemo kutoka England, Cameroon pia Indonesia.
Baada ya
kucheza soka nchini baadaye Uarabuni, Masatu aliondoka nchini na kwenda
Indonesia ambako alicheza soka kwa zaidi ya miaka mitano kabla ya kustaafu na
baadaye akapata kazi katika shule ya watoto iliyo chini ya klabu maarufu ya
England ya Arsenal ambako alifanya kazi kwa miaka mitatu na ushee.
Masatu
anasema sasa amerejea nyumbani Tanzania baada ya kuishi Indonesia kwa zaidi ya
miaka nane na atafanya nini?
“Kuna mambo
mengi sana ya kufanya, lakini tunaweza kuzungumza kwanza masuala ya soka na
baadaye, nitawaeleza mambo yatakavyokuwa na kipi ambacho nimepanga kukifanya,”
anasema Masatu katika mahojiano yake ya kwanza na gazeti la Championi ikiwa ni
siku moja tu baada ya kutua nchini.
Kesho,
Masatu ataelezea kuhusiana na mambo mengi ya maisha yake. Usiache kufuatilia
kupitia blog hii ya wanamichezo na wapenda burudani…







0 COMMENTS:
Post a Comment