July 17, 2013


OGBU (WA TATU KUTOKA KUSHOTO MWENYE JEZI YA NIGERIA), AKIWA KATIKA MAZOEZI YA YANGA LEO CHINI YA KOCHA ERNIE BRANDTS.

 Mshambuliaji aliyetua Jangwani kuanza majaribio, Brendan Ogbu ,20, kutoka Nigeria leo asubuhi ameanza mazoezi na timu hiyo.

Ogbu anayekipiga katika timu ya Heartland ya Nigeria ameonyesha uwezo mzuri mazoezini na Kocha Mkuu, Ernie Brandts amesisitiza kuwa kweli ataanza mechi ya kesho dhidi ya timu ya Wanigeria wenzake.



Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pillars FC ya Nigeria ambayo inaundwa na wachezaji kutoka timu mbalimbali. Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mazoezi ya leo, Ogbu alionyesha uwezo mkubwa wa kupiga mashuti, kuiwahi mipira mashuti na kuwa kivutio.


Mashabiki wa Yanga watamshuhudia kesho kwa mara ya kwanza akionyeshana kazi na mabeki Wanigeria wa Pillars FC na Yanga watakuwa na nafasi ya kuamua kuhusu kumsajili au la.

1 COMMENTS:

  1. nna wasiwasi na huyo mchezaji kama kweli katoka heartland kwani heartland ni timu kubwa yanga wawe makini anaweza akawa naye ni feki kama three pillars na ameletwa na wakala gani au kajileta mwenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic