Pamoja na majigambo ya Kocha David Moyes kwamba mshambuliaji wake Wayne Rooney hataondoka, taarifa zinaeleza Rooney ameweka msisitizo kuwa antaka kuondoka.
Rooney amesisitiza anataka kuondoka Manchester United akionyesha pia kukerwa na kauli za mara kwa mara za Moyes ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Everton.
Hivi karibuni, Moyes aliviambia vyombo vya habari kwamba Rooney hataondoka na hiyo ilikuwa ni baada ya kukutana na kufanya mkutano wa wawili.
Kwa mujibu wa Sky Sports, Rooney anajiona hana kitu kipya au kigeni anachoweza kukifanya Manchester United kwa kuwa amefanya kila kitu katika miaka tisa aliyokuwa hapo.
Rooney alikaa saa 24 tu katika ziara ya United nchini Thailand kabla ya kurejeshwa England baada ya kuumia.
Alishaandiska barua kwa klabu hiyo na kueleza anataka kuondoka, lakini Moyes amekuwa akijaribu kumbakiza.
Lakini inaonekana Rooney aliyetokea Everton na kutua United anaonekana hana raha na mbaya zaidi amekuwa akikumbuka mashabiki wa United waliomzomea wakati alipolinua juu kombe la ubingwa wa Ligi Kuu England.








0 COMMENTS:
Post a Comment