NGASSA AKIWA MAZOEZINI JANA NA KIKOSI CHA STARS JIJINI KAMPALA, KULIA NI DAVID LUHENDE NA KUSHOTO FRANK DOMAYO |
Wakazi
wa jiji la Kampala nchini Uganda wamekuwa wakimzungumzia zaidi kiungo mwenye
kasi wa Taifa Stars, Mrisho Khalfan Ngassa huku wakimfananisha na winga wa
zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila ambaye jina lake ni kubwa sana jijini humo.
Kwenye
mitaa yenye mikusanyiko ya watu jijini Kampala na Entebbe hasa maeneo ya Soko
Owino, Kisenyi na Namirembe wamekuwa wakijadili kuhusiana na mechi ya leo ya
Kombe la Chan na Ngassa ndiye gumzo kwa Tanzania.
Wengi
wamekuwa wakizungumza namna The Cranes watakavyofanya kazi ya ziada kumzuia
Ngassa ambaye anajulikana kwa kuwa na kasi kubwa.
Mashabiki
hao wamekuwa wakimzungumzia mchezaji wepesi na kasi yake uwanjani na jinsi
anavyoutumia mwili vizuri wake mdogo kupenya na mpira kwenye msitu wa mabeki na
kufanya mashambulizi kwa kupachika mabao au kumpasia mtu wa kumalizia.
"Yule Murisho Mugasa ni hatari
sana yule Mugasa, yaani jinsi vile anacheza ni kama yule mlikuwa mnamuita
Lunyamila alivyokuwa akitutesaga pale kwenye uwanja wetu wa zamani wa
Nakivubo" alisema mmoja wa Waganda aliyezungumza blogu hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment