| ...Lulu |
Kampuni
ya Wananchi Group kupitia huduma yake ya Zuku, imetoa zawadi ya tuzo na fedha kwa
wasanii wa filamu za Kiswahili zilizoshinda kwenye Tamasha la Filamu la Kimataifa
Zanzibar (Ziff).
Wasanii
hao akiwemo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu walikabidhiwa zawadi hizo mbele
ya waandishi wa habari kwenye ofisi za Zuku, Morocco jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kampuni hiyo, Ali Mafuruki aliwataja washindi wa tuzo hizo kuwa ni Lulu
aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike kupitia filamu yake ya Woman of
Principle.
Halafu
Bond Bin Suleiman aliyetwaa tuzo tatu, Muigizaji Bora, Muongozaji Bora na Mtunzi
Bora.
| ...Amir Shivji |
Mwingine
ni Amir Shivji ambaye filamu yake ya Shoe Shine iliyoongoza kupendwa wengi. Tuzo
hizo zilienda sambamba na kitita cha shilingi laki tano kila moja.
Mafuruki
aliwataka wananchi kujipatia ving’amuzi vya Zuku kwa bei nafuu ambapo wataweza
kuona chaneli zaidi ya 85 zenye muonekano mzuri bila kusahau chaneli ya filamu
za Kiswahili.
Zuku
ina ving’amuzi vya aina mbalimbali ambavyo vimekuwa vikipendwa na watu wengi
zaidi kutokana na kuwa na chaneli bora za filamu, michezo, muziki, habari.







0 COMMENTS:
Post a Comment