Straika wa West Ham, Andy Carroll,
juzi usiku alionyesha kuwa ni mtu wa kujali watu wengine baada ya kumkabidhi
ombaomba pauni 50 ambazo ni zaidi ya shilingi 130,000.
Carroll ambaye alikuwa majeruhi kwa
muda, alimpa fedha hiyo ombaomba huyo ambaye alimsogelea karibu wakati
alipokuwa ndani ya Jiji la London, England.
Msimu uliopita, mshambuliaji huyo
alikuwa akichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Liverpool ambapo alishindwa
kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kiwango chake kutokuwa cha
kuridhisha. Hatimaye West Ham ikamsajili rasmi.
.jpg)
.jpg)








0 COMMENTS:
Post a Comment