Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
amesisitiza kuwa ataendelea kumuwania mshambuliaji wa Manchester United, Wayne
Rooney mpaka sekunde ya mwisho ya usajili wa safari hii.
Rooney amekuwa akitajwa kuwaniwa na
Chelsea lakini klabu yake imekataa ofa mbili zilizotolewa na Chelsea
inayomuwania kwa nguvu.
Uamuzi wa kocha huyo raia wa Ureno
umekuja wakati ambapo Kocha wa Man United, David Moyes akisisitiza kuwa hana
mpango wa kumuuza Rooney ambaye ana umri wa miaka 27.
“Tulipeleka ofa na Manchester United
wakakataa, tusubiri kitakachotokea, tunafanya mambo kisheria, hatujazungumza na
mchezaji kwa kuwa kila kitu kinakwenda kwa utaratibu.
“Tuna washambuliaji wazuri lakini
tutaendelea kuwamia mpaka siku ya mwisho,” alisema Mourinho ambaye pia
amesisitiza kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza beki David Luiz kwenda
Barcelona.








0 COMMENTS:
Post a Comment