Huku akiwa
amevaa jezi ya Simba, Juma Kassim ‘Nature’ au Kiroboto alikamua vilivyo leo
katika tamasha la Simba Day.
Akiwa na
kundi la Wanaume Halisi, pembeni Omary wa Mabaga Fresh pia Tunda Man, burudani
ilikuwa ya nguvu.
Burudani
ilikuwa ya aina yake, huku Nature akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa
Msimbazi.
Nature ni
shabiki mkubwa wa Yanga na amekuwa akifanya shoo nyingi zinazoihusisha Yanga.
Lakini safari
hii uongozi wa Simba ukaangalia suala la msanii yupi mwenye mashabiki wengi na
Nature akaangalia kazi yake bila ya kutanguliza ushabiki hivyo kufanya burudani
katika Simba Day kuwa ya kutosha.







safiiii
ReplyDelete