Simba wameila
vizuri Simba Day baada ya kuwatwanga wageni wao SC Villa ya Uganda kwa mabao
4-1.
SC Villa ndiyo
timu iliyomlea kiungo nyota wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye amejiunga
na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Katika mechi
hiyo, SC Villa ilianza kupata bao katika dakika ya 8 lililofungwa na 8 kupitia
kwa Robert Mganga na Jonas Mkude akaisawazishia Simba katika dakika ya 43.
Kipindi cha pili
timu hizo zilicheza soka la kasi na kupaniana zaidi lakini Simba walikuwa wenye
njaa zaidi ya mabao baada ya kuzitikisa nyavu za SC Villa mara tatu.
Mabao mawili
yalifungwa na mshambuliaji wake mpya, Betram Mombeki aliyefunga mawili na
Lucian William ‘Gallas’.
KIKOSI CHA SIMBA
LEO:
Abel Dhaira,
Masoud Nassor ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Miraji Adam,
Jonas Mkude, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Amri
Kiemba & Haruna Chanongo.
Kabla ya mechi
hiyo, Twalipo walifanikiwa kuwafunga Simba B kwa mabao 6-3.







0 COMMENTS:
Post a Comment