![]() |
| RAIS WA TFF, LEODEGER CHILLA TENGA |
Mchakato wa uchaguzi wa kamati mpya
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa
kesho (Agosti 13 mwaka huu).
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF
saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza
tarehe mpya ya uchaguzi huo ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka
huu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana
Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na inatarajia kuwa na kikao kingine leo (Agosti
12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya
uchaguzi huo.
Mbali ya Mbwezeleni, wajumbe wengine
wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga
Dyamwale na Kitwana Manara.








0 COMMENTS:
Post a Comment