Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inakutana leo jioni (Agosti
13 mwaka huu) na kesho (Agosti 14 mwaka huu) kupitia na kufanyia uamuzi usajili
wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya kwanza ya usajili
imeshamalizika wakati hatua ya pili ya usajili inaanza kesho (Agosti 14 mwaka
huu) ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya
Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania.
Hivyo, dirisha la uhamisho kwa
wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika
Agosti 29 mwaka huu








0 COMMENTS:
Post a Comment