Kiungo mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba, amesema kikosi chao
kipo tayari kwa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013/2014.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kiemba alisema kikosi chao
kipo tayari na mashabiki hawatakiwi kuwa na hofu juu ya hilo na sasa
wanapigania kuhakikisha wanatwaa ubingwa.
Alisema licha ya kuwa na matatizo madogomadogo, anaamini kocha
atayafanyia kazi na ligi ikianza tu wataona moto wao.
“Timu yetu ipo tayari kushiriki ligi na tutapigana ili kuhakikisha
tunatwaa ubingwa kwa kuwa tunashiriki kwa ajili hiyo tu,” alisema Kiemba.







0 COMMENTS:
Post a Comment