Kocha Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts, amesema uwezekano wa beki huyo ni mdogo kutokana na kuwa majeruhi.
Timu hizo
zinatarajiwa kuvaana Jumamosi ijayo katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
Championi Jumatano, Brandts alisema beki huyo amekaa nje ya uwanja kwa wiki
mbili bila mazoezi, hivyo ni ngumu kwake kutoa maamuzi ya kucheza au kutocheza.
Brandts alisema
beki huyo ameanza mazoezi juzi Jumatatu, hivyo ataendelea kuangalia maendeleo
yake katika mazoezi ingawa jambo la kucheza kwenye mechi hiyo ni gumu sana.
“Hatima ya Mbuyu
ya kucheza au kutocheza katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam bado sijaijua.
“Ameanza mazoezi mepesi
na wenzake, ni mapema kutangaza kuwa atacheza au hatacheza, ninaendelea
kumuangalia kujua kama yupo fiti au vipi,” alisema Brandts.







0 COMMENTS:
Post a Comment