Wanamichezo 25 wamechukua fomu
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Fomu hizo zilianza kutolewa juzi
(Agosti 16 mwaka huu) ambapo wawili wamechukua nafasi ya Rais na wengine wawili
Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji
wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa
kuwa wagombea urais ni Jamal Malinzi na Omari Musa Nkwarulo wakati umakamu wa
rais hadi sasa umewavutia Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Waliochukua fomu za ujumbe ni
Athuman Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella,
Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe na
Khalid Mohamed.
Wengine ni Muhsin Balhabou, Omari
Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir
Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu
aliyechukua fomu mpaka sasa ni Hamad Yahya anayeomba kuteuliwa kugombea nafasi
ya uenyekiti.
Fomu za maombi pia zinapatikana
kupitia tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni ya Agosti 20 mwaka
huu.
Fomu zikiambatanishwa na risiti ya
malipo (receipt) au malipo ya benki (deposit slip) kupitia akaunti ya TFF namba
01J1019956700 iliyoko CRDB tawi la Holland House zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa
TFF kwa mkono au kwa barua pepe (email) ambayo ni tanfootball@tff.or.tz
0 COMMENTS:
Post a Comment