Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii
(Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2013/2014 iliyochezwa
jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
208,107,000. Washabiki 26,084 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo
ilimalizika kwa Yanga kushinda Azam bao 1-0.
Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo
uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama
ya tiketi sh. 7,309,866.
Uwanja sh. 22,236,194.76, gharama za
mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 5,188,445.44, TFF sh. 13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.
0 COMMENTS:
Post a Comment