Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho ameahidi ataendelea kumfuatilia na kutaka kumsajili
mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney.
Mourinho
amesema ataendelea kufanya hivyo hadi dirisha la usajili litakapofungwa.
“Baada
ya hapo itajulikana kama tumefanikiwa kumsajili au la, lakini ni mchezaji
ambaye tunamhitaji na Chelsea ni sehemu mwafaka kwake,” alisema Mourinho.
Jana,
Mourinho aliiongoza Chelsea kuanza msimu vizuri kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya Hull City.
Mourinho
amekuwa akiendeleza juhudi zake za kumnasa Rooney ambaye anaonekana kutokuwa na
maisha mazuri ndani ya Man United.
Hata
hivyo, Rooney alicheza katika mechi kati ya Man United dhidi ya Swansea na
kutoa basi za mabao mawili yaliyozaa ushindi wa 4-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment