Beki Rio Ferdinand ameambiwa
hataruhusiwa kutumia mechi ya hisani ya timu yake kwa ajili ya kutangaza nembo
ya bidhaa zake kwenye kipute cha timu yake ya Manchester United dhidi ya
Seville, leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Mechi hiyo ambayo itashuhudiwa na
zaidi ya mashabiki 50,000 itachezwa kwa ajili yake katika kusherekea kutimia
miaka 10 ya uwepo wake klabuni hapo.
Watu wa masoko wa United walikaa
kikaa na wale wa upande wa beki huyo ambapo baada ya majadiliano marefu
waliamua kuwa Ferdinand, 34, hatakiwi kutumia mechi hiyo kuipromoti nembo ya
bidhaa zake binafsi inayotambulika kwa kusomeka kama namba 5 (#5).
Mara kadhaa Rio amekuwa akionekana
amevaa fulana, kofia na vingine vikiwa na alama hiyo ambayo inawakilisha
biashara zake kadhaa nje ya soka.
Lakini wakati uamuzi huo unafanyika,
imeelezwa kuwa umechekewa kwa kuwa kuna vipeperushi na nembo kadha zenye alama
ya #5 ambazo nyingi zilikuwa zimeshasambazwa kwa mashabiki.
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment