Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemwandikia Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi ili kufanya uamuzi wenye manufaa kwa washabiki wa mpira wa
miguu baada ya tarehe ya uchaguzi aliyotangaza kuingilia na mechi ya watani wa
jadi (Simba na Yanga) ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Leo, Salehjembe iliandika kuhusiana na kushangazwa na uamuzi wa TFF
kukubali uchaguzi wake mkuu kufanyika siku moja na mechi kubwa ya Ligi Kuu Bara
katika ya Simba na Yanga Oktoba 20.
Sekretarieti ya TFF imepokea maoni kutoka kwa wapenzi mbalimbali wa
mpira wa miguu wakiomba matukio hayo mawili (Uchaguzi wa TFF na mechi ya Simba
na Yanga) yafanyike katika siku tofauti.
Wakati Kamati ya Uchaguzi inatangaza uchaguzi kufanyika Oktoba 20 mwaka
huu tayari ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa imeshatoka, na ikionesha kuwa
timu ambazo zina historia ya kipekee katika mpira wa miguu zitacheza siku hiyo.
Sekretarieti imelazimika kumwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
kwa vile yeye na kamati yake ndiye wenye mamlaka ya kuitisha Mkutano wa
Uchaguzi. Huko nyuma TFF imeshafanya mikutano huku kukiwa na mechi za timu ya
Taifa (Taifa Stars), jambo ambalo liliwezekana kutokana na mikutano hiyo kuwa
na ajenda moja tu.
Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni ameitisha
kikao cha kamati yake kujadili barua hiyo ya sekretarieti.
0 COMMENTS:
Post a Comment