Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu
cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa
TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.
Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni
kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli
nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana
kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.
Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa
Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa
viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa
na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti
24 mwaka huu.
Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa
Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.
Kamati imesema inaamini wahusika
wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu
utakaosababishwa na mabadiliko hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment