Na Wilbert Molandi
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Husseni Javu
amepewa jezi namba 21 ambayo ilikuwa ikitumiwa na kiungo mshambuliaji wa
kimataifa wa timu hiyo, Mrundi, Didier Kavumbagu.
Javu alijiunga na Yanga hivi karibuni na
kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar ya
Manungu mkoani Morogoro.
Akizungumza na Championi Ijumaa, meneja wa
timu hiyo, Hafidh Saleh alisema Kavumbagu hataivaa tena namba hiyo, badala yake
msimu ujao wa ligi ataonekana akivaa na jezi namba saba ambayo ilikuwa
ikitumiwa na Nizar Khalfan.
Saleh alisema kiungo wao mshambuliaji mpya,
Mrisho Ngassa aliyetokea Simba amepewa namba tisa iliyokuwa ikivaliwa na Omega
Seme aliyepelekwa kwa mkopo Tanzania Prisons.
“Kavumbagu hataonekana akivaa jezi namba 21
kwenye msimu ujao na badala yake ataonekana akivaa namba saba,” alisema Saleh.








Kavumbagu alianza kuvaa namba 7.raundi ya pili ya ligi kuu ilipoanza msimu ulopita na hata alipoifunga simba alikuwa amevaa namba 7.
ReplyDelete