Kiungo Mtanzania, Mwinyi Kazimoto amecheza Ligi Daraja la Pili nchini Qatar kwa mara
ya kwanza, tena kwa dakika 90, lakini bahati mbaya timu yake ya Al Markhiya
imeambulia kipigo cha mabao 2-1.
Akizungumza kutoka jijini Doha, Kazimoto alisema wameanza mechi ya kwanza kwa kipigo
lakini wanatarajia kujirekebisha katika mechi nyingine watakayocheza kesho
Jumamosi.
“Tumeanza kwa
kupoteza, kidogo timu nazisahau majina. Lakini tuna mechi nyingine ya ligi
Jumamosi, hii itakuwa ni ya pili. Tuna timu nzuri tu kwa kweli, kuhusiana na
kucheza namshukuru Mungu kwa kuwa ninapata nafasi, nimecheza namba nane kwa
dakika zote 90 na nilicheza vizuri.
“Kupata namba
haikuwa rahisi lakini nimejituma na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema
Kazimoto alipokuwa ‘akigonga’ stori moja kwa moja na Championi Ijumaa.
Kiungo huyo
wa zamani wa Simba alijihakikishia namba wakati wa mechi za kirafiki ambazo
aling’ara na kocha wake akaamua kumpa ‘dimba la juu’ ahangaike nalo.







0 COMMENTS:
Post a Comment