Kiwango kikubwa alichokionyesha kiungo
mkabaji wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’ kimesababisha amwagiwe ‘minoti’ na
mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, juzi.
Kiungo huyo mkongwe akitokea benchi
akichukua nafasi ya chipukizi, Frank Domayo, alionyesha kiwango kikubwa kiasi
cha kuwashawishi mashabiki wa timu hiyo kabla ya kuanza kumshangilia.
Mkongwe huyo alitumia uwezo na uzoefu
wake kutawala safu ya kiungo kwenye mchezo huo, ambayo hapo awali ilitawaliwa na
kiungo chipukizi wa wapinzani wao, Hassani Dilunga.
Tukio hilo la kutunzwa fedha, lilitokea
mara baada ya mechi hiyo kumalizika na Yanga kushinda 1-0.
Championi Jumatatu lilishuhudia Chuji
akipewa Sh 30,000 na mashabiki alipokuwa akitoka uwanjani na kuingia kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo akipita karibu na jukwaa lililokuwa na mashabiki
wa Yanga.
Alipoulizwa
kiungo huyo kuhusiana na pongezi hizo, alisema: “Ujue mtu mzima dawa siku zote,
kama ulivyoona ni ngumu kukielezea kiwango changu, mashabiki ndiyo wanaona
ndani ya uwanja, nafikiri mwenyewe umewaona.”
0 COMMENTS:
Post a Comment