Huku akiwa kambini Manungu, Morogoro, vibaka
wamevamia nyumba ya mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa Mgosi na kuiba baadhi
ya vitu kwenye gari. Nyumba hiyo ipo jijini Dar.
Kiungo huyo alikuwa kambini mkoani huko
kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ashanti
United iliyotarajiwa kuchezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Manungu.
Mgosi amesema kundi hilo la vibaka, lilivamia nyumbani kwake Yombo jijini Dar usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita na kuvunja gari aina ya Alteza na kuiba vioo ‘side mirror’ na ‘power window’ zote.
Mgosi alisema hiyo ni mara ya pili kwa
vibaka hao kuruka na kuiba, mara ya kwanza walivamia na kuiba vitu hivyo kwenye
gari ya mkewe aina ya Nadia, hivyo alipanga kuwasaka mara baada ya kumaliza
mechi dhidi ya Ashanti.
“Ndugu yangu nipo huku kambini Manungu
nikijiandaa na mechi ya ligi dhidi ya Ashanti, lakini nimeshtushwa na taarifa
za kuvamiwa nyumbani kwangu na kuibiwa baadhi ya vitu vya gari langu aina ya
Alteza.
“Kiukweli nimechukizwa na kitendo hiki,
hiyo ni mara ya pili kwa vibaka hao kuruka ukuta na kuiba, mara ya kwanza
waliruka ukuta na kuiba side mirror na power window kama nilizoibiwa mimi,
hivyo nimepanga kuwatafuta mara baada ya mechi ya Jumapili (jana) dhidi ya
Ashanti,” alisema Mgosi kwa masikitiko.
0 COMMENTS:
Post a Comment