WAMBURA |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Eliud Mvella amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi uliopangwa
kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura amesema, Mvella amemwandikia
barua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni akielezea
uamuzi wake huo pamoja na mambo mengine umetokana na kile alichodai kuwa Kamati
hiyo haikumtendea haki kwa kumwondoa.
Mbwezeleni amekiri kupokea barua hiyo, na kuongeza kuwa licha ya
uamuzi huo wa Mvella aliyekuwa ameomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji
kupitia Kanda Namba Saba ya mikoa ya Iringa na Mbeya, bado suala lake
litasikilizwa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.
Kamati ya Mbwezeleni ilimuondoa Mvella katika kinyang’anyiro hicho
kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective
responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya Utendaji
ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye muhtasari na
baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa.
0 COMMENTS:
Post a Comment