September 30, 2013





Uchezaji wa kibabe wa Ruvu Shooting na kiwango kidogo walichoonyesha Yanga, kulisababisha Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kumuita muuza lambalamba za Bakhresa.


Baada ya kumuita, Manji alitoa fedha mfukoni na kununua lambalamba moja halafu akaanza kuifungua taratibu.



Hata kabla hajamaliza, mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Lloyd Nchunga alijitokeza, wakafanya mazungumzo kidogo yaliyoashiria kujadili uchezaji wa timu yao siku hiyo.


Hadi mapumziko ilikuwa ni sare ya bila kufungana na Yanga ilishindwa kuonyesha kiwango kama kile katika mechi dhidi ya Azam FC, siku chache zilizopita.

Baada ya dakika chache za mazungumzo na Nchunga, Manji alijipumzisha katika kiti chake na kuendea kutoa ‘stress’ na lambalamba yake, taratiiibu.

Jamaa mmoja aliyekuwa upande wa kulia wa jukwaa la VIP alilokuwa Manji, alionyesha kushangazwa na mwenyekiti huyo milionea kula lambalamba.

“Manji ameonyesha si mpenda makuu, lakini ameonyesha hana kinyongo na Bakhresa kama ambavyo imekuwa ikikuzwa wakati wa suala la haki za TV. Si unaona anakula bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic