April 26, 2019


BAADA ya Jana kushindwa kuumudu mchezo kati ya KMC na Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewapiga pini waamuzi hao kwa kuchezesha mchezo huo chini ya kiwango.

Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mabao 2-1 huku wakipewa penalti mbili ambayo moja ilikoswa na Meddie Kagere na ya pili ikafungwa na John Bocco uwanja wa CCM Kirumba.

(TFF), imewaondoa kwenye orodha ya waamuzi wa msimu huu, Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro ambao walichezesha mchezo huo wa KMC na Simba jana Aprili 25, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirikisho hilo, waamuzi hao wameondolewa kuchezesha mechi zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo Kambuzi alikuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Godfrey Msakila na mwamuzi msaidizi namba mbili Consolata Lazaro.

Katika taarifa hiyo, TFF imewaonya waamuzi wote wa ligi kuu, ligi daraja la kwanza na daraja la pili kuwa makini “Yeyote atakayebainika kuchezesha chini ya kiwango kwa namna yoyote atachukuliwa hatua stahiki”, imeeleza taarifa hiyo.

21 COMMENTS:

  1. Hata wakisimamishwa lengo lao lishatimizwa; Simba apate Pointi 3, hii kwa kweli ni janja ya nyani kula hindi bichi!! KMC walioonewa wanapata fidia gani, Azam aliyeshushwa nafas moja anapata ahueni gani?
    Nyie waachieni waendelee tu soka letu tushalizoea wenyewe. Hadi pesa za Mo zirudi.
    Wabillah taufiq

    ReplyDelete
  2. Naona hii habari kama haijasomwa bado na wanasimba........

    ReplyDelete
  3. hicho kikao kimekaa saa ngapi na leo ni siku ya mapumziko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nahoji pia msingi wa maamuzi maana hienda hata report ya kabisa bado

      Delete
  4. Vikao vya kuhusu mechi za Simba vinakaa siku hiyo hiyo.Kwenye mechi zingine hata akipigwa Refa itapita miezi 2 bila hatua kuchukuliwa .Mechi ya Yanga na Prisons alipigwa Refa hatua gani zilichukuliwa?
    Na bado mapoyoyo wanadai Simba inabebwa!Mechi ya kwanza Yanga na Simba refa,alikataa goli la halali la Okwi. Alichukuliwa hatua?
    Hasara ya pointi 2 za Simba alilipa nani?
    Chezeni mpira .Msitafute mchawi.

    ReplyDelete
  5. Nani anasimamia ligi?TFF au Bodi ya ligi?Ndimbo anahusika vipi na
    adhabu za marefa? MBONA MAREFA WENGI WAMEBORONGA!WHY NOW?

    ReplyDelete
  6. Madogo nao walimnawisha mtyu et mpira umefuata mkono cc xoka letu ndo lilivyowandugu hata msojali wacha nae atesetese kidogo kiukwel kiwango alichokionesha simba toka na coastal, Kagera, Alliance na Kmc wakawaida sanaaa bc tyu miundombinu inafanya yake nakumbuka enz hizo had simba ikiitwa Malalamiko fc Leo wanavyobebwa kimyaaaaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. tunaosema kiwango walichoonyesha SImba kwa coastal, Kagera na Alliance ni kawaida moja ya sababu ni kwa kuwa Simba inacheza ugenini..TP Mazembe ni timu bora Africa mbonna hapa Dar walikuwa wa kawaida?..hivyo hivyo pia kwa Nkana na Al Ahly na AS Vita.Kuna faida ya kuchezea uwanja wa nyumbani..Tuache Siasa! Je ni kiwango kipi Yanga amekuwa anaonyesha hadi kuwa kileleni mwa ligi..Amekuwa anashinda kwa bahati na wote tunajua huwezi bahatisha kila siku ndio kinachotokea sasa kwa Yanga. Alikuwa Anapata point tatu lakini anazidiwa ball possession, .Mchezo wake ni wa pasi ndefu za kushtukiza na kuvizia ziwakute washambuliaji wafunge.Na hapo anachezea DaR!Je hicho ndio kiwango bora?.Anashinda tuseme ni kwa bahati, 1-0, 2-1 na mara nyingi zaidi ya asilimin 60 goli la kuongoza linapatikana dakika ya 70, au 80 muda ambao sio rafiki kurudisha goli.Unajua Yanga ameteleza wapi ?Ni kwa sabbat hivi sasa anacheza nje ya Dar?Hivyo hata Simba kama wamecheza chini ya kiwango inaeleweka ni kwa sababu hawachezei uwanja wa kwa Mkapa!Ni kwa kiwango hafifu hicho hicho ndio Simba alifika 8 bora...Tutumie busara je hiyo ratiba ya mechi 5 siku kumi ni rafiki kuonyesha kiwango bora?Inabidi kocha abadili wachezaji kila mechi au kiwango kingekuwa hovyo zaidi.Hiyo badili badili inashusha kiwango

      Delete
  7. Kikao kilichokaa na kutoa adhabu ni kipi?Bodi ya ligi inaendeshwa na mihemko ya mashabiki?

    ReplyDelete
  8. Waliitwa malalamiko FC kwanini?Kila mechi ya Simba na Yanga mchezaji wa Simba alionyeshwa kadi nyekundu.Magoli ya mkono.Wachezaji kucheza wakiwa na kadi 3 za njano huku Malinzi akilazimisha rufaa zitupwe.KARMA.

    ReplyDelete
  9. Kama ni penalt ni penalt tu kosa la refa lipo wapi?

    ReplyDelete
  10. HIYO NDIO TFF AMBAO WENGINE WANASEMA ETI INAWAPENDELEA SIMBA? INAWAPENDELEAJE ? WENYEWE TUU HAWANA UWEZO WA KAZI. KIKAO KILIPASWA KIFANYIKE KUFIKIA UAMUZI HUO. MIMI NAKUBALI NILIONA UDHAIFU WA MWAMUZI NA 2 OFFSIDE ALIOWANYIMA GOLI AMBALO SIMBA WALIKUWA WALIPATE MWANZONI TU MWA MCHEZO UKWELI HAIKUWA OFFSIDE HATA KOCHA WA KMC ALIBAKIA KUCHEKA. LAKINI MIPIRA YA KUCHEZA NA MKONO NI TAFSIRI YA SASA AMBAYO SASA FIFA ITAIFUTA HAND TO BALL NA BALL TO HAND IPI UMEONA? HUWEZI LAUMU REFA KWENYE TAFSIRI HII.

    ReplyDelete
  11. Bongo tunacheza mpira mdomoni. Ndio maana kila tunaepangwa nae kimataifa tunaona kundi la kifo kumbe sisi ndio tuliokufa. Fifa ianzishe mashindano ya majungu tutabeba kombe

    ReplyDelete
  12. Mpira wetu unaharibiwa na ushabiki wa Simba na Yanga....hii ndiyo sumu ya kuua mpira wa Tanzania

    ReplyDelete
  13. Hii haisaidii ktk soka maana kuwafungia waamuzi haibadilisha maumivu kwa timu uliyoonewa na kipoteza haki yao ktk dakika 90, pia inashangaaza kuona walioshinda wanafurahia kwa matokeo ya figisu figisu, hii ligi TFF munajiosha kwa maji yenye tope kuweni wavumilivu kma tunavyoona dalili zote, na kusubiria muliemtayarishia ubingwa mumkabidhi kwa wakati munaopenda, ila tutabaki nyuma kimaendeleo kunahaja ya kubadilika kiusimba na kiuyanga na kuongoza kwa haki na kuepuka majungu na upangaji matokeo

    ReplyDelete
  14. Hebu weka wazi na utoe mfano ni haki gani iliyonyimwa KMC?

    ReplyDelete
  15. Enzi za Malinzi wanayanga tulifurahi. Sasa ni zama zingine. Walipolalamika wengine tuliwabeza nä kuwapa majina ohh nendeni FIFA leo kibao kimegeuka tumesahau.

    ReplyDelete
    Replies
    1. saluti kwako, kilchobaki wallace karia ale kiapo kwenye utawala wke yanga hawez kuwa bingwa, na manara aje na zle tv atuoneshe

      Delete
  16. kwaani kibaya kipi kutoa penait 2 au simba sc kushinda,kama timu imeushika mpira ndani ya box adhabu yake nin kama matuta na haijalishi kaunawa Mara ngapi!

    ReplyDelete
  17. penalty huwa na utata mara nyingi..kuna maamuzi tata ya offside, rafu aliyofanya Juuko..Huwenda ndiyo sababu ya waamuzi kusimamishwa na TFF, sio latiam zile penalty..Kama mtu akinawa ndani ya penalt box, adhabu ni penalt...Ndiyo huyo mlinzi ajifunze kukaba akiwa ameficha mikono yake nyuma..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic