Imeelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa
zamani wa Simba, Emmanuel Okwi anadaiwa kuwagawa viongozi wa timu hiyo
inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Okwi aliihama Simba katikati ya msimu
uliopita na kutua Etoile du Sahel ya Tunisia lakini amekuwa akitajwa kurejea
nchini kujiunga na Simba kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na klabu yake,
ikidaiwa kuwa ni kutokana na masuala ya malipo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo
zinaeleza kuwa, Okwi amekuwa akionyesha nia ya kurejea Simba, huku baadhi ya
viongozi wakiwa hawamtaki na wengine wakitaka arejee kwa madai kuwa tangu
aondoke, pengo lake uwanjani halijazibika.
“Okwi anaomba mwenyewe kurudi
kuichezea Simba, lakini ni ngumu kwake kutokana na rekodi ya nidhamu yake kutokuwa
nzuri. Hivyo, hadi hivi sasa bado haijulikani kama atarudi au hatarudi, hilo
walifikia muafaka baada ya viongozi hao kukubaliana,” kilisema chanzo.
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba,
Ezekiel Kamwaga kuhusiana na taarifa hizo, alisema: “Suala hilo ni gumu kwangu
kulijibu, linahusu viongozi wangu wa juu ikiwemo kamati ya usajili.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment