Uongozi wa Yanga umemzungumzia Patrick Naggi na
kusema si aliyechukua nafasi ya katibu mkuu badala yake alikwenda ‘kutalii’.
Katika mkutano na waandishi wa habari leo, Makamu wa
Rais wa Yanga, Clement Sanga alisema Naggi ni kati ya wale wanaowania uongozi.
“Naggi hajaaliliwa na kuna kampuni ya uwakala ambayo
inafanya mchakato wa kupatikana kwa katibu mkuu. Naggi ni kati ya wanaowania.
“Yeye aliamua kufika klabuni kama kutalii hivi ili
kuona mazingira, hakuna kiongozi ambaye tayari amezungumza naye kwa kuwa kazi
hiyo inafanywa na kampuni ya uwakala ambayo siwezi kuitaja.
“Mchakato ukikamilika, basi tutaelezwa na kamati ya
utendaji itakaa, tukikubaliana jina litatangazwa,” alisema Sanga.
Hata hivyo, kulionekana kuna hali ya mkanganyiko
kidogo kwa kuwa Naggi aliingia hadi ofisini na kuanza kuzungumza mambo kadhaa
muhimu ya ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako.
Mwalusako aliomba kuongoza Yanga kwa muda wa mwaka
mmoja ambayo umekamilika, lakini imeelezwa ataendela na kazi hadi hapo
atakapopatikana huyo mpya.
Naggi aliyewahi kuwa mkurugenzi wa ufundi wa
Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) alitimuliwa na wazee wa Yanga ambao walidai
kushangazwa na ujio wake wa kushtukiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment