KASEJA (MWENYE KOFIA) AKIFUATILIA MECHI YA JANA UWANJA WA TAIFA. MBELE YAKE MWENYE NYWELE ZENYE RANGI NI UHURU SELEMANI |
Katika kipindi cha miaka kumi sasa, kipa
wa zamani wa Simba, Juma Kaseja aliingia kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa
kama shabiki.
Kaseja aliyekuwa nahodha wa Simba,
aliachwa katika kikosi hicho kwa madai ya kushuka kiwango ingawa kila kitu
kinaonyesha zilikuwa ni chuki binafsi.
Katika mechi ya jana iliyomalizika kwa
sare ya mabao 3-3, Kaseja alionyesha vitu kadhaa muhimu ambavyo vinaweza
kuelezewa.
Pamoja na kuachwa kwa chuki binafasi,
lakini alionyesha hana chuki na Simba na kwenda kukaa katika jukwaa la
mashabiki wa Simba.
Achana na hivyo, Kaseja alizidi
kuonyesha yeye ni Simba damu kwa kuwa kama ingekuwa tofauti angeweza kwenda
kukaa jukwaa la Yanga aliyowahi kuichezea kwa mwaka mmoja.
Tatu, akiwa na Uhuru Selemani ambaye pia
aliwahi kuichezea Simba, Kaseja alionekana si mpenda makuu kwani alikaa sehemu
ya kawaida na akaonyesha utulivu si kama walivyo wachezaji wengine nyota.
Wakati Simba ikishindiliwa mabao katika
kipindi cha kwanza alionekana kama alikuwa anawaza kitu fulani, angalau katika
kipindi cha pili, tabasamu lake lilianza kuonekana.
0 COMMENTS:
Post a Comment