Kama ilivyotazamiwa kwamba lazima kutakuwa na namna katika suala la mapato, kwamba Simba na Yanga zimeingiza Sh milioni 500 tu!
Tiketi za mechi hiyo ziliisha mapema, lakini mashabiki waliingia hadi wakakaa kwenye ngazi za kupitia, maana yake watu walikuwa wengi kuzidi viti vya uwanjani.
Lakini ripoti kutoka TFF imeeleza namba hii, anza kuisoma;
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa jana
(Oktoba 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare
ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000.
Washabiki
57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Ni
tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya
VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi
ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.
Kila
klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh.
7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh.
37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.
0 COMMENTS:
Post a Comment