October 21, 2013


Uongozi wa Coastal Union ya Tanga umemalizana na kocha Hemed Morocco kwa kumueleza “basi”.


Coastal imemkabidhi barua Morocco kwamba haitamuongezea mkataba baada ya aliokuwa nao kumalizika.

“Wamenipa barua, lakini mkataba wangu pia uliisha na tulikuwa katika mazungumzo.

“Kuna vitu sikufurahia na huenda walijua nisingeweza kuongeza. Maana wakati wakiniita tuzungumze, msemaji wa klabu aliishasema nimefukuzwa.


“Hii ilinichanganya kidogo na ndiyo maana sikupenda kuendelea Coasta. Ila vizuri tumemalizana,” alisema Morocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic