October 14, 2013

BABA UBAYA (WA PILI KUSHOTO) AKIJIFUA NA KIKOSI CHA SIMBA B, LEO



Beki wa kushoto wa Simba, Issa Rashid amerejea mazoezini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili.


Rashid maarufu kama Baba Ubaya, leo amefanya mazoezi na kikosi cha Simba B chini ya Kocha wake, Selemani Matola.
Baba Ubaya alijumuika na vijana wa Simba na kufanya mazoezi makali ya kukimbia.

Matola alisema ameungana nao ili kutafuta fitness kwa kuwa alikaa nje ya uwanja kutokana na maumivu.

Pamoja na kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki moja na ushee, Baba Ubaya alionyesha juhudi kubwa na kuwa mmoja ya waliofanya vizuri katika mazoezi hayo ya kukimbia kwa muda mrefu.

Katika mechi nne ilizocheza, Simba imetumia mabeki watatu tofauti wa kushoto na yote hiyo ni kutokana na kuumia kwa Baba Ubaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic