Kocha Mkuu wa Simba B, Selemani Matola
ameonyesha hataki utani na kikosi chake baada ya kuendelea na mazoezi makali
licha ya kuwa ni Nyerere Day.
Salehjembe imeshuhudia Matola akiendelea
kuwapa mazoezi makali vijana wake.
Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Mwenye
Shooting jijini Dar, vijana hao walikuwa wakizunguka uwanja wakionyesha wazi
wamechoka lakini Matola na Meneja wake, Patrick Rweymamu walionekana hawataki
mzaha.
Moja ya vikosi bora vya timu ya vijana
ni hicho cha Simba na kimekuwa kikionyesha soka la kuvutia.
Matola alisema: “Tunatambua leo ni
sikukuu ya kuadhimisha miaka 14 ya Mwalimu Nyerere, lakini ilikuwa lazima
tufanye mazoezi asubuhi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment