Kundi la mashabiki wanaodaiwa kuwa wa
Simba, juzi Jumamosi lilitanda nje ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
likimsubiri Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ili kumwambia aondoke
katika timu hiyo.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya mechi
ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Ruvu Shooting kumalizika kwa sare ya
bao 1-1.
Blogu hii ilishuhudia kundi hilo la
mashabiki likiwa kwenye geti kuu la kuingilia Uwanja wa Taifa, likikagua kila
gari iliyokuwa inatoka ili kumnasa Julio.
Mashabiki hao walisikika wakimtuhumu
kocha huyo kwamba ndiyo chanzo cha timu yao kufanya vibaya na kuiharibu kwa
makusudi.
Kundi hilo la mashabiki lilijaribu kulizunguka
gari la waandishi wa Championi na kuomba wamfikishie ujumbe Julio kwamba
awaachie Simba yao chini ya Abdallah Kibadeni.
Pia mashabiki walilifuata gari aina ya
Mazda Merrina la kiungo mkabaji wa timu hiyo, Abdulhalim Humud wakimsifia na kuhoji
sababu ya kuwekwa benchi wakati ana uwezo mkubwa. Baadaye polisi waliwavamia na
kuwatawanya.
“Tunaomba mumfikishie ujumbe Julio, hatumtaki,
aondoke zake, anatuharibia timu yetu. Amuachie Kibadeni aendelee nayo,”
alisikika mmoja wa mashabiki hao.
mwisho
0 COMMENTS:
Post a Comment