Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni, bado
hajajua ampange nani kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kati ya kiungo
Jonas Mkude na Abdulhalim Humud.
Siku 10 ambazo ni saa 240 zinatosha kwa kocha huyo mkongwe kujua ampange nani kati yao.
Kibadeni amekuwa akiwabadilisha viungo
hao wakabaji mara kwa mara ili kutafuta mmoja atakayekuwa chaguo la kwanza, lakini
mpaka sasa hajampata na amesisitiza baada ya mechi kumi atakuwa ameshapata
kikosi cha kwanza akiwemo mchezaji mmoja kati ya Humud na Mkude.
Kibadeni amesema kuwa viungo hao viwango vyao havipishani, hali inayompa shida kuchagua mmoja.
Kibadeni alisema viungo hao wote wana ‘kontroo’,
nguvu na pasi zao ni nzuri.
“Kama unakumbuka kwenye mechi iliyopita
dhidi ya JKT Ruvu kiungo wangu Humud alianza na Mkude hakukaa benchi kabisa.
“Katika mechi ya juzi dhidi ya Ruvu Shoting,
Mkude alianza na Humud alikaa benchi, lengo langu ni kuangalia uwezo wa kila
mmoja ndani ya uwanja nikiwa natafuta kikosi cha kwanza imara.
“Nadhani baada ya mechi kumi nitakuwa
nimepata kikosi changu cha kwanza,” alisema Kibadeni ambaye msimu uliopita
aliifundisha Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment