Ghana imejiweka katika nafasi
nzuri ya kucheza Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil baada ya kuwaadhibu Misri
kwa mabao 6-1.
Kipigo hicho cha aina yake
kimetokea muda mchache uliopita kwenye Uwanja wa Baba Yara mjini Kumasi na ni
kikubwa zaidi kwa vigogo hao wa Afrika kuwahi kukipata.
Asamoah Gyan alifunga bao maoja dakika
ya tano kabla ya kutoa pasi kwa Mubarak Wakasso katika dakika ya 52.
Nyota Mohammed AbouTreika ndiye alifunga bao pekee na
Misri na ikaonekana kama amewapa hasira zaidi Ghana ambao walifunga mabao yao
mengine kupitia kwa Sulley Muntari na Cristian Atsu aliyeingia kipindi cha
pili.
Ghana walionekana kuutawala zaidi mchezo, huku nahodha wao
Michael Essien na Muntari wakitawala katika sehemu ya kiungo.
Inaonekana kama Ghana imeshavuka kwani ni nadra kwa Misri kupata
ushindi wa mabao 5-0, lakini Essien amesema hawawezi kuwabeza wapinzani wao
hata kidogo kabla ya kujihakikishia katika mechi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment