Mshambuliaji wa Manchester
United, Luis Nani ameiongoza timu yake ya taifa ya Ureno kuibabua Luxemburg kwa
mabao 3-0.
Mechi hiyo ya kuwania kucheza
Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil ilikuwa na upinzani mkubwa.
Awali ilionekana kuwa Ureno
imepania baada ya kuona nafasi inazidi kuwa finyu kwani mechi iliyopita
ilimaliza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Israel.
Mabao katika mechi ya leo
yalifungwa na Silvestre Varela, Nani akatupiala pili na mkali Helder Postiga
akamalizia kazi.
Nani alikuwa msaada mkubwa
kutokana na krosi zake lakini alikuwa tishio kwa mabeki wa wenyeji wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment