KIBADENI (KUSHOTO) AKIWA NA MEMBA WOTE WA BENCHI LA UFUNDI |
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho
(Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Kocha Abdallah Kibadeni aliyeinoa Kagera msimu uliopita, atakuwa akikutana nayo kwa mara ya kwanza akiwa na timu tofauti ambayo ni Simba.
Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa
moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu
katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na
mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga),
Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu
Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers
(Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3
mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa
kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu
vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting,
Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza
na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment