October 22, 2013







Kocha Salum Baus wa Zanzibar Heroes amewaacha wachezaji kadhaa maarufu kama nadir Haroub 'Cannavaro', Agrey Morris na Abdi Kassim 'Babi'.


Wachezaji watakaounda timu hiyo na timu zao kwenye mabano ni walinda milango Mwadini Ali Mwadini (Azam fc), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting) na Ali Suleiman Abdi (KMKM) wakati walinzi ni Mohammed Azan ‘Brown’ (Polisi - Zanzibar), Waziri Salum (Azam ), Shafii Hassan (Malindi) na Mohammed Faki (Zimamoto).

Wengine katika nafasi hiyo ni Salum Haji Juma (Miembeni), Said Yussuf (Mtende Rangers), Mohammed Othman Mmanga (Jamhuri), Mussa Said Magarawa (Chwaka Stars) na Nassor Masoud ‘Cholo’ (Simba).

Viungo wa timu hiyo ni pamoja na Abdulhalim Humuod (Simba), Sabri Ali Makame (Oljoro JKT), Adeyoum Saleh (Simba) na Is-haka Othman (JKU).

Wengine ni Ali Kani Mkanga (JKT Ruvu), Hamadi Mshamata (Chuoni), Hamadi Juma Issa na Masoud Ali Mohammed (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji katika kikosi hicho ni Seif Abdalla Rashid na Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ wa Azam, Suleiman Kassim Suleiman ‘Solembe’ (Coastal Union), Amour Omar Mohammed ‘Janja’ (Miembeni) na Amir Omar Hamad (Oljoro JKT).

Wachezaji wengine katika safu ya ushambuliaji ni Jaku Joma Jaku (Mafunzo), Faki Nahoda (Kimbunga F. C), Hassan Seif Ali (Mtibwa) na mfungaji bora wa mashindano ya kombe copa cola yaliyomalizika hivi karibuni Juma Ali Yussuf anaechezea timu ya New Vission inayoshiriki ligi daraja la central wilaya ya Mjini, Unguja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic